Jumanne, 18 Juni 2019

Wimbo wa Dini | 48. Mungu Anashuka na Hukumu

48. Mungu Anashuka na Hukumu

I
Anapokuja chini katika taifa la joka kuu jekundu,
Mungu anageuka kuutazama ulimwengu na unaanza kutingika.
Je, kuna mahali popote ambapo hapatapata hukumu Yake?
Ama kuishi katika janga Analotoa?
Kila mahali Aendapo anamwaga mbegu ya janga,
lakini kupitia kwayo Anatoa wokovu na kuonyesha upendo Wake.
Mungu anatamani kuwafanya watu zaidi kumjua, kumwona na kumheshimu.
Hawajamwona kwa muda mrefu, lakini sasa Yeye ni wa kweli kabisa.

Jumatatu, 17 Juni 2019

Matamshi ya Mungu | Kazi na Kuingia (9)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Tamaduni za asili na mitazamo ya kiakili madhubuti vimeweka kivuli katika roho safi na ya kitoto ya mwanadamu, vimeshambulia roho ya mwanadamu bila ubinadamu hata kidogo kana kwamba anaondolewa hisia na hali yoyote ya nafsi. Mbinu za mashetani hawa ni za kikatili kupita kiasi, na ni kana kwamba “elimu” na “malezi” vimekuwa ni njia za kitamaduni ambazo kwazo mfalme wa mashetani anamchinja mwanadamu; kwa kutumia “mafundisho yake ya kina” anafunika kabisa roho yake mbaya, akivaa mavazi ya kondoo ili kupata imani ya mwanadamu na halafu kusubiri mwanadamu akiwa amelala na kummeza kabisa.

Jumapili, 16 Juni 2019

Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” Sehemu ya Nne



Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” Sehemu ya Nne

Mwenyezi Mungu anasema, “Hapa tunasoma kuyahusu maneno yale halisi yaliyozungumzwa na Ayubu, maneno ambayo ni thibitisho kwamba alikuwa amemshinda Shetani. Alisema: ‘Nilitoka kwa tumbo la mama yangu nikiwa uchi, na mimi nitarudi huko nikiwa uchi.’ Huu ndio mwelekeo wa utiifu ambao Ayubu anao kwa Mungu. Kisha, akasema: ‘Yehova alinipa, na Yehova amechukua; jina la Yehova libarikiwe.’ Maneno haya yaliyozungumzwa na Ayubu yanathibitisha kwamba Mungu anaangalia kina cha moyo wa binadamu, kwamba Anaweza kuangalia kwenye akili ya binadamu, na yanathibitisha kwamba kuidhinisha kwake kwa Ayubu hakuna kosa, kwamba binadamu huyu aliyeidhinishwa na Mungu alikuwa mwenye haki. 

Jumamosi, 15 Juni 2019

Neno la Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” Uendelezo wa Sehemu ya Nne



Neno la Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” Uendelezo wa Sehemu ya Nne


Mwenyezi Mungu anasema, “Wakati Ayubu alipopitia majaribio yake kwa mara ya kwanza, alinyang’anywa mali yake yote na watoto wake wote, lakini hakujisujudia na kusema chochote ambacho kilikuwa dhambi dhidi ya Mungu kutokana na hayo. ... Kwenye jaribio la pili, Shetani aliunyosha mbele mkono wake ili kumdhuru Ayubu, na ingawaje Ayubu alipitia maumivu yaliyokuwa makubwa zaidi kuliko yale aliyokuwa amepitia awali, bado ushuhuda wake ulikuwa wa kutosha wa kuacha watu wakiwa wameshangazwa. 

Ijumaa, 14 Juni 2019

Maneno ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV Utakatifu wa Mungu (I)” Sehemu ya Pili



Maneno ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV Utakatifu wa Mungu (I)” Sehemu ya Pili


Mwenyezi Mungu anasema, “Mungu anafanya kazi, Mungu anamtunza mtu, anamwangalia mtu, na Shetani anafuata hatua Yake yote. Yeyote anayefadhiliwa na Mungu, Shetani pia anatazama, akifuata nyuma. Iwapo Mungu anamtaka mtu huyu, Shetani atafanya kila kitu kwa uwezo wake kumzuia Mungu, akitumia mbinu mbalimbali mbovu kujaribu, kusumbua na kuharibu kazi anayofanya Mungu ili kufikia lengo lake lililofichwa. 

Alhamisi, 13 Juni 2019

Wimbo wa Injili "Mwana wa Adamu Ameonekana" | Sifu Kurudi kwa Yesu Mwokozi | Watoto Wanacheza Ngoma



Wimbo wa Injili "Mwana wa Adamu Ameonekana" | Sifu Kurudi kwa Yesu Mwokozi | Watoto Wanacheza Ngoma

Kutoka Mashariki ya ulimwengu (Mashariki ... Mashariki ...),
mwale wa mwanga unatokea (mwanga ... mwanga ...),
ukiangaza njia yote kwenda magharibi.
Mwana wa Adamu ameshuka duniani.

Mwokozi amerejea, Yeye ni Mwenyezi Mungu.
Akionyesha ukweli, Ameanzisha enzi mpya.
Mwana wa Adamu ameonekana. (Siyo?)
Mungu amekuja. (Eh!)
Yeye huwaletea binadamu njia ya uzima wa milele (njia ya uzima wa milele).

Jumatano, 12 Juni 2019

“Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV)” Sehemu ya Nne


Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee X Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV)” Sehemu ya Nne
Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”. Maudhui ya video hii: Mahitaji ya Mungu kwa Wanadamu 1. Utambulisho na Hadhi ya Mungu Mwenyewe 2. Mielekeo Mbalimbali ya Wanadamu kwa Mungu 3. Mwelekeo Ambao Mungu Anahitaji Mwanadamu Awe Nao Kwake
Yaliyopendekezwa: App ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Jumanne, 11 Juni 2019

Matamshi ya Mungu | Kazi na Kuingia (8)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu


Nimezungumza mara nyingi sana kwamba kazi ya Mungu ya siku za mwisho ni kwa ajili ya kubadilisha roho ya kila mtu, kubadilisha nafsi ya kila mtu, ili kwamba moyo wake, ambao umeteseka sana na kiwewe, uwe umebadilishwa, hivyo kuokoa nafsi yake, ambayo imeumizwa kwa kina zaidi na uovu; ni kwa sababu ya kuamsha roho za watu, kuyeyusha mioyo yao baridi, na kuwaruhusu kurudisha nguvu za ujana. Haya ndiyo mapenzi makubwa ya Mungu.

Jumatatu, 10 Juni 2019

Neno la Mungu | Kazi na Kuingia (7)

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu
Imemchukua mwanadamu mpaka siku hii kutambua kwamba kile mtu anachokosa si tu kuruzukiwa maisha ya kiroho na uzoefu wa kumjua Mungu, lakini, muhimu zaidi, mabadiliko katika tabia yake. Kutokana na ujinga kamili wa mwanadamu wa historia na utamaduni wa kale wa wanadamu, hana ujuzi wa kazi ya Mungu hata kidogo. Mwanadamu hutumaini kuwa ndani kabisa ya moyo, mwanadamu anaweza kumpenda Mungu sana, lakini kwa sababu ya upotovu mkubwa mno wa mwili wa mwanadamu, pamoja na kutojali na upumbavu, mwanadamu ameshushwa kuwa asiye na ufahamu wa Mungu hata kidogo. 

Jumapili, 9 Juni 2019

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | "Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake"



Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho | "Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake"

Mwenyezi Mungu anasema, “Hakuna mtu mbali na Yeye anayeweza kujua mawazo yetu yote, au kufahamu asili yetu na kiini chetu kwa dhahiri na ukamilifu, ama kuhukumu uasi na upotovu wa binadamu, ama kusema nasi na kufanya kazi kati yetu kama hivi kwa niaba ya Mungu aliye mbinguni. Hakuna mtu isipokuwa Yeye ambaye amepewa mamlaka, hekima, na heshima ya Mungu; tabia ya Mungu na kile Mungu Anacho na alicho yanatoka, kwa ukamilifu wao, ndani Yake. Hakuna mtu mbali na Yeye ambaye anaweza kutuonyesha njia na kutuletea mwangaza.

Jumamosi, 8 Juni 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII” Sehemu ya Kwanza



Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VII ” Sehemu ya Kwanza

Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”.
Maudhui ya video hii:
Mhutasari wa Mamlaka ya Mungu, Tabia ya Haki ya Mungu, na Utakatifu wa Mungu

Ijumaa, 7 Juni 2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V Utakatifu wa Mungu II” Sehemu ya Nne


      Mwenyezi Mungu anasema, “Kuelewa kiini cha Mungu na kujua kiini cha Mungu kinapeana msaada usioweza kupimika kwa kuingia kwa watu katika maisha. Natumai kwamba hamtapuuza haya ama kuyaona kama mchezo; kwa sababu kumjua Mungu ni msingi muhimu na msingi wa imani ya mwanadamu kwa Mungu na ufuatiliaji wa mwanadamu wa ukweli na wokovu na kitu ambacho hakifai kuachiliwa. Iwapo mwanadamu anamwamini Mungu lakini hamjui Mungu, na iwapo mwanadamu anaishi miongoni mwa baadhi ya barua na mafundisho ya kidini, hutawahi kufikia wokovu hata kama utatenda na kuishi kulingana na maana ya juujuu ya ukweli. Hiyo ni kusema, iwapo imani yako kwa Mungu haitokani na kumjua, basi imani yako haimaanishi chochote.

      Yaliyopendekezwa: App ya Kanisa la Mwenyezi Mungu