Matamshi ya Mwenyezi Mungu | Kazi na Kuingia (1)
Tangu watu waanze kuikanyaga njia sahihi ya maisha, kumekuwa na mambo mengi ambayo bado hayajaeleweka vizuri. Bado wapo kwenye mkanganyiko kabisa kuhusu kazi ya Mungu, na kuhusu kiasi gani cha kazi wanapaswa kufanya. Hii, kwa upande mmoja, ni kwa sababu ya kuwa na uelekeo tofauti wa uzoefu wao na mipaka katika uwezo wao wa kupokea; kwa upande mwingine, ni kwa sababu kazi ya Mungu bado haijawaleta watu katika hatua hii.
