Jumanne, 13 Novemba 2018

Kuendeleza Ubora wa Tabia ni Kwa Ajili ya Kupokea Wokovu wa Mungu


Kuendeleza Ubora wa Tabia ni Kwa Ajili ya Kupokea Wokovu wa Mungu


Mwenyezi Mungu anasema, "Kuendeleza ubora wa tabia ya watu kunahitaji kwamba muendeleze uwezo wenu wa kupokea. Hitaji la msingi kabisa kwenu ni kwamba myapokee waziwazi maneno yanayonenwa kwenu. Je, siyo imani iliyovurugika ikiwa unanifuata bila kufahamu kile Ninachosema? Ubora wenu wa tabia ni duni sana. Ni kwa sababu hammiliki uwezo wa kupokea kwamba hamna ufahamu hata mdogo wa kile kinachosemwa. Kwa hivyo, ni vigumu sana kutimiza matokeo yanayotamanika.

Jumatatu, 12 Novemba 2018

Umeme wa Mashariki | Tamko la Sitini na Mbili


Umeme wa Mashariki | Tamko la Sitini na Mbili

Kuyaelewa mapenzi Yangu hakufanywi ili tu kwamba uweze kujua, ila pia kwamba uweze kutenda kulingana na nia Yangu. Watu hawauelewi moyo Wangu. Ninaposema huku ni mashariki, wanalazimika kuenda na kutafakari, wakijiuliza, “Kweli ni mashariki? Pengine sio. Siwezi kuamini kwa urahisi hivyo. Nahitaji kujionea mwenyewe.” Ninyi watu ni wagumu sana kushughulikia, na hamjui utii wa kweli ni nini.

Jumapili, 11 Novemba 2018

Filamu za Kikristo 2018 | "Kumbukumbu Chungu" | Welcoming the Return of the Lord in Judgement



Fan Guoyi alikuwa mzee wa kanisa la nyumba kule Uchina. Wakati wa zaidi ya miaka ishirini ya huduma, siku zote alimwiga Paulo, na kufanya kazi kwa bidii na akamtumikia Bwana kwa shauku kubwa. Aidha, alisadiki kabisa kwamba katika kufuata imani yake kwa njia hii, alikuwa akitenda mapenzi ya Baba wa mbinguni, na kwamba wakati Bwana angerudi, angenyakuliwa kwa hakika na kuenda kwenye ufalme wa mbinguni. 

Jumamosi, 10 Novemba 2018

Muziki wa Injili "Umuhimu wa Mungu Kumsimamia Binadamu" | God Is Salvation to Man



Muziki wa Injili "Umuhimu wa Mungu Kumsimamia Binadamu" | God Is Salvation to Man


Usimamizi wa Mungu ni ili kuwapata binadamu
wanaomwabudu na kumtii Yeye.
Ingawa wamepotoshwa na Shetani, hawamwiti baba tena.
Wanajua ubaya wa Shetani, hivyo wanamkataa.
Wanakuja mbele ya Mungu, wanakubali adabu na hukumu.
Wanajua kile kilicho kibaya, na kile ambacho ni kitakatifu.
Na wanajua ukuu wa Mungu, na uovu wa Shetani.
Jamii kama hii ya binadamu haitamfanyia Shetani kazi wala kumwabudu tena.
Kwa sababu hawa ni watu ambao kwa kweli wametwaliwa na Mungu.
Hii ndiyo sababu Mungu anamsimamia mwanadamu.

Ijumaa, 9 Novemba 2018

Umeme wa Mashariki | Tamko la Nane


Kwa kuwa Mwenyezi Mungu—Mfalme wa ufalme—ameshuhudiwa, mawanda ya usimamizi wa Mungu yamejitokeza kabisa katika ulimwengu wote. Sio tu kwamba kuonekana kwa Mungu kumeshuhudiwa nchini China, lakini jina la Mwenyezi Mungu limeshuhudiwa katika mataifa yote na nchi zote. Wote wanaliita jina hili takatifu, wakitafuta kufanya ushirika na Mungu kwa njia yoyote iwezekanayo, wakiyafumbata mapenzi ya Mwenyezi Mungu na kuhudumu kwa uratibu katika kanisa. Roho Mtakatifu hufanya kazi kwa njia hii ya ajabu. 

Alhamisi, 8 Novemba 2018

Swahili Christian Variety Show | "Kuwa Katika Hali Ngumu" (Crosstalk) | Christian Testimony of Overcoming Satan



Mazungumzo chekeshi haya, Kuwa Katika Hali Ngumu, yanasimulia hadithi ya Geng Xin , afisa wa Kikomunisti wa China ambaye ameikubali kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho. Inasimulia uzoefu wake wa kupoteza kazi yake, kukamatwa, na kuadhibiwa kwa ukatili na CCP kwa sababu ya imani yake, na mwishowe kwake kuwa shahidi kwa Mungu. Hili linaonyesha shida za Wakristo nchini China na linaonyesha mfano halisi wa imani na ushupavu wa Wakristo kumtegemea Mungu ili kumshinda Shetani, na kushuhudia.

Jumatano, 7 Novemba 2018

Nyimbo ya Msifuni Mwenyezi Mungu | 85. Umo Moyoni Mwangu



                                       85. Umo Moyoni Mwangu                              



     I
Ninapotenda wajibu wangu mbali na nyumbani,
nawaza kukuhusu, na ninakuomba.
Kupitia kusoma maneno Yako,
nimekuja kukuamini zaidi na moyo wangu unapozwa, oo.
Kukushuhudia Wewe, ninapitia machungu mengi,
na najua hata vizuri zaidi jinsi Unavyopendeza.
Kukufuata, nitatembea milele hadi mwisho.
Unapobadilisha umbo Lako,
tutakaribisha kurudi Kwako, ee,
tutakaribisha kurudi Kwako.

Jumanne, 6 Novemba 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Tamko la Kumi na Mbili

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Tamko la Kumi na Mbili


Ikiwa una tabia ambayo si thabiti, nyepesi kuhamaki kama upepo au mvua, kama huwezi kuendelea kusonga mbele, basi fimbo Yangu haitakuwa mbali na wewe. Unaposhughulikiwa, kadiri hali ilivyo mbaya zaidi, na kadiri unavyoteswa zaidi, ndivyo upendo wako kwa Mungu unavyoongezeka, na unaacha kushikilia dunia. Bila njia nyingine, unakuja Kwangu, na unapata tena nguvu na imani yako. Ilhali, katika hali rahisi, ungeboronga. Ni lazima uingie ndani kwa mtazamo chanya, uwe mwenye vitendo na si baridi. Hutatingisika na yeyote na chochote katika hali yoyote, na huwezi kushawishiwa na maneno ya yeyote.

Jumatatu, 5 Novemba 2018

Filamu za Kikristo "Kumbukumbu Chungu" | Ni Vigezo Vipi vya Kuingia Kwenye Ufalme wa Mbinguni?


     
Kuhusiana na ni mtu aina gani anayeweza kuingia kwenye ufalme wa mbinguni, Bwana Yesu alisema, "ila yule atendaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni" (Mathayo 7:21). Kwa hivyo ni mtu aina gani hasa anayefanya mapenzi ya Baba wa mbinguni? Watu wengi husadiki kwamba wale wanaofuata mfano wa Paulo na kufanya kazi kwa uangalifu na bidii nyingi kwa ajili ya Bwana ndio wanaofanya mapenzi ya Baba wa mbinguni.

Jumamosi, 3 Novemba 2018

Umeme wa Mashariki | Tamko la Tisa


Umeme wa Mashariki | Tamko la Tisa


Nataka kukukumbusha kwamba huwezi kuwa na wasiwasi hata kidogo juu ya neno Langu na kutokujali kwa aina yoyote hakukubaliki. Unapaswa kulisikiliza na kulitii na kutenda mambo kulingana na nia Zangu. Daima lazima uwe macho na kamwe usiwe na tabia ambayo ni ya kiburi na ya kujidai, na lazima kila wakati unitegemee Mimi ili kutupilia mbali tabia ya zamani ya asili ambayo hukaa ndani yako. 

Swahili Gospel Movie Segment "Mungu Anashikilia Ukuu Juu Ya Majaliwa ya Kila Nchi na Watu Wote"




Swahili Gospel Movie Segment "Mungu Anashikilia Ukuu Juu Ya Majaliwa ya Kila Nchi na Watu Wote"

Milki ya kale ya Kirumi na Milki ya zamani ya Uingereza zilikuwa na mafanikio na nguvu kwa haraka sana na kisha kufifia kuelekea kudhoofika na uharibifu. Sasa, Marekani limekuwa taifa kubwa lisilobishaniwa la ulimwengu na pia lina jukumu lisilofidika la kudumisha na kuimarisha hali ya ulimwengu. Ni mafumbo ya aina gani hasa yaliyofichika kuhusiana na kuinuka na kuanguka kwa mataifa? Ni nani aliye na mamlaka juu ya majaliwa ya kila nchi na watu wote? Sehemu hii ya ajabu kutoka kwa filamu ya Kikristo, "Yule Anayeshikilia Ukuu Juu ya Kila Kitu", itakufichulia majibu haya.

Ijumaa, 2 Novemba 2018

Tamko la Saba

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Tamko la Saba


Kuinuka kwa mazingira pande zetu zote huharakisha kurudi nyuma kwetu katika roho. Usitende kwa moyo mgumu, usipuuze kwa vyovyote vile kama Roho Mtakatifu Ana wasiwasi, usijaribu kuwa mjanja na usiwe na ridhaa kupita kiasi na kuridhika kibinafsi au kuzingatia sana matatizo yako mwenyewe; kitu pekee cha kufanya ni kumwabudu Mungu katika roho na kweli. Huwezi kuyaacha maneno ya Mungu nyuma au kuyapa kisogo; lazima uyaelewae kwa makini, rudia kuomba-kusoma kwako, na uelewe maisha ndani ya maneno hayo.