Neno la Mwenyezi Mungu | Tamko la Thelathini na Tatu
Ufalme Wangu unawahitaji wale ambao ni waaminifu, wasio wanafiki, na wasio wadanganyifu. Je, si watu wenye moyo safi na waaminifu duniani hawapendwi na watu? Mimi ni kinyume kabisa cha jinsi ilivyo. Inakubalika kwa watu waaminifu kuja Kwangu; Nafurahia mtu wa aina hii, pia Ninamhitaji mtu wa aina hii. Hii ni haki Yangu hasa. Watu wengine ni wajinga; hawawezi kuhisi kazi ya Roho Mtakatifu na hawawezi kuyaelewa mapenzi Yangu. Hawawezi kuona familia yao na hali zinazowazingira kwa uwazi, wanafanya vitu bila kufikiri na kupoteza fursa nyingi za neema.
