Jumatano, 31 Oktoba 2018

Tamko la Sita


Mwenyezi Mungu, Mkuu wa vitu vyote, hushika madaraka Yake ya kifalme kutoka kwa kiti Chake cha enzi. Yeye hutawala ulimwengu na vitu vyote Naye Anatuongoza katika dunia yote. Mara kwa mara tutakuwa karibu Naye, na kuja mbele Zake kwa utulivu; kamwe hatutakosa wakati mmoja, na kuna mambo ya kujifunza wakati wote. Mazingira yanayotuzunguka pamoja na watu, mambo na vitu, yote yameruhusiwa na kiti Chake cha enzi. Usiwe na moyo wa kunung’unika, au Mungu hatatupa neema Yake juu yako.

Jumanne, 30 Oktoba 2018

Onyo kwa Wale Wasioweka Ukweli katika Vitendo


Onyo kwa Wale Wasioweka Ukweli katika Vitendo



Mwenyezi Mungu anasema, "Wale miongoni mwa ndugu na dada ambao daima hueneza ubaya wao ni vibaraka wa Shetani na hulivuruga kanisa. Watu hawa lazima siku moja wafukuzwe na kuondolewa. Katika Imani yao kwa Mungu, ikiwa watu hawana moyo wa kumcha Mungu ndani yao, ikiwa hawana moyo ambao ni mtiifu kwa Mungu, basi hawatashindwa tu kufanya kazi yoyote ya Mungu, lakini kinyume na hayo watakuwa watu wanaovuruga kazi ya Mungu na wanaomuasi Mungu.

Jumatatu, 29 Oktoba 2018

"Kumbukumbu Chungu" | Nini Hasa Ni Uhusiano Kati ya Kuokolewa na Kuingia kwenye Ufalme wa Mbinguni?



Filamu za Kikristo "Kumbukumbu Chungu" | Nini Hasa Ni Uhusiano Kati ya Kuokolewa na Kuingia kwenye Ufalme wa Mbinguni?

Watu wengi wanasadiki kwamba kwa kumsadiki Bwana Yesu dhambi zao zinasamehewa, kwamba wanaokolewa kupitia kwa imani, na zaidi kwamba pindi mtu anapookolewa anaokolewa milele, na pindi Bwana anaporudi ananyakuliwa na kuingia kwenye ufalme wa mbinguni! Ilhali Bwana Yesu alisema, "Si kila mtu aniitaye, Bwana, Bwana, ataingia katika ufalme wa mbinguni; ila yule atendaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni" (Mathayo 7:21).

Jumapili, 28 Oktoba 2018

Uhusiano Wako Na Mungu Ukoje


Uhusiano Wako Na Mungu Ukoje



Mwenyezi Mungu anasema, "Katika kuwa na imani kwa Mungu, ni lazima angalau utatue swala la kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu. Bila uhusiano wa kawaida na Mungu, basi umuhimu wa kumwamini Mungu unapotea. Kuunda uhusiano wa kawaida na Mungu kunapatikana kikamilifu kupitia kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu.

Jumamosi, 27 Oktoba 2018

Filamu za Kikristo | “Kumbukumbu Chungu” Movie Clip: Wokovu Kupitia Imani Pekee Unaweza Kuwa Tiketi ya Kuingia Katika Ufalme wa Mbinguni?


Filamu za Kikristo | “Kumbukumbu Chungu” Movie Clip: Wokovu Kupitia Imani Pekee Unaweza Kuwa Tiketi ya Kuingia Katika Ufalme wa Mbinguni?


Hasa ni mtu aina gani anayeweza kuingia kwenye ufalme wa mbinguni? Baadhi ya watu hufikiria dhambi zetu zinasamehewa pindi tunaposadiki Bwana, kwamba pindi tunapookolewa basi tunaokolewa milele, na kwamba mtu aina hii anaweza kunyakuliwa na kuingia kwenye ufalme wa mbinguni. Kisha kuna wale wanaosadiki kwamba, ingawa dhambi zetu zinasamehewa pindi tunaposadiki Bwana, bado tunafanya dhambi mara kwa mara na hatujafikia utakatifu, na kwa sababu Biblia inasema kwamba wale ambao si watakatifu hawawezi kumwona Bwana, basi ni vipi tunaweza kunyakuliwa na kuingia kwenye ufalme wa mbinguni wakati hatujafikia utakatifu? Hivyo ni nani aliye sahihi na nani asiye sahihi kutokana na mitazamo hii miwili? Tafadhali tazama pande zote mbili zikishiriki katika majadiliano makali!

Ijumaa, 26 Oktoba 2018

Tamko la Sitini na Nane


Tamko la Sitini na Nane



Mwenyezi Mungu anasema, "Neno Langu linatekelezwa katika kila nchi, mahali, taifa na kikundi, na neno Langu linakamilishwa katika kila pembe wakati wowote. Maafa yanayotokea kila mahali si vita kati ya watu, wala si mapigano na silaha. Hakutakuwa na vita tena baadaye. Wote wako katika mfumbato Wangu. Wote watakabili hukumu Yangu na watadhoofika kati ya maafa. Acha wale wanaonipinga na wale wasioanza kushirikiana na Mimi wateseke uchungu wa maafa mbalimbali. 

Alhamisi, 25 Oktoba 2018

Swahili Gospel Choir Song "Ufalme" | New Jerusalem Has Come Down Out of Heaven


 Ufalme

Ufalme, mji wa watakatifu, ufalme wa Kristo.
Katika ufalme, utajiri na utukufu wa Mungu hudhihirishwa.
Umeme unatoka Mashariki na kuangaza hadi Magharibi.
Mwanga wa kweli uko hapa, neno la Mungu limeonekana katika mwili.
Mwokozi amesharudi, akishuka juu ya wingu jeupe.
Watakatifu leo ​​wamenyakuliwa mbele ya kiti cha enzi ili kumwabudu Mungu.

Jumatano, 24 Oktoba 2018

Swahili Christian Skit | "Baba Yangu, Mchungaji" | A Debate on the Bible in a Family




 Chi Shou, mchungaji wa dini ambaye amekuwa muumini wa Bwana kwa miaka arubaini, daima ameshikilia mitazamo kwamba "maneno na kazi yote ya Bwana yako ndani ya Biblia," na kwamba "imani katika Bwana haiwezi kuacha Biblia, na kuiamini Biblia humaanisha kumwamini Bwana." Inapojulikana kwamba binti yake ameikubali kazi ya Mungu ya siku za mwisho, anafanya mpango na mke wake kumkomesha. Katika siku hii, binti yao anarudi nyumbani kushuhudia injili ya kurudi kwa Bwana, na mjadala mkali, mcheshi, ilhali mzito wa familia unatokea ...

     Kuhusu Sisi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Jumanne, 23 Oktoba 2018

Umeme wa Mashariki | Ufafanuzi wa Tamko la Thelathini na Tano

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

Umeme wa Mashariki | Ufafanuzi wa Tamko la Thelathini na Tano

Siku hizi, binadamu wote, kwa viwango vinavyotofautiana, wameingia katika hali ya kuadibu. Kama tu alivyosema Mungu, “Naenda mbele na binadamu sako kwa bako.” Hii ni kweli kabisa, lakini watu bado hawawezi kulielewa kabisa wazo hili. Kutokana na hili, sehemu ya kazi ambayo wamefanya imekuwa si lazima. Mungu alisema, “Mimi husaidia na kuwaruzuku kwa mujibu wa kimo chao. 

Jumatatu, 22 Oktoba 2018

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Tamko la Nne

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Tamko la Nne
Watu Wangu wote wanaohudumu mbele Zangu wanapaswa kutafakari kuhusu siku zilizopita: Je, upendo wenu Kwangu ulikuwa umetiwa doa na uchafu? Je, uaminifu wenu Kwangu ulikuwa safi na wa moyo wako wote? Je, ufahamu wenu kunihusu ulikuwa wa kweli? Je, Nilikuwa na nafasi kiasi gani katika nyoyo zenu? Je, Nilikuwa Nimejaza nyoyo zenu zote? Je, maneno Yangu yalitimiza kiasi gani ndani yenu? Msinichukue kama mpumbavu!

Jumapili, 21 Oktoba 2018

Swahili Gospel Video Clip "Maangamizi ya Mungu ya Sodoma na Gomora"



Swahili Gospel Video Clip "Maangamizi ya Mungu ya Sodoma na Gomora"


Ikifurika na uovu na uzinzi, miji hii miwili mikubwa ya Sodoma na Gomora iliichokoza tabia ya Mungu. Mungu alinyesha moto wa jahanamu kutoka mbinguni, akiiteketeza hiyo miji na watu ndani yayo hadi kuwa majivu, na kuwafanya watoweke katikati ya hasira Yake…. Tazama dondoo ya filamu ya Kikristo Maangamizo ya Mungu ya Sodoma na Gomora ili kujua zaidi juu ya tabia ya ghadhabu, isiyokiukwa ya Mungu na onyo Lake kwa vizazi vijavyo.

    Kuhusu Sisi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Jumamosi, 20 Oktoba 2018

Umeme wa Mashariki | Tamko la Tatu

Umeme wa Mashariki | Tamko la Tatu

Mfalme wa ushindi hukaa juu ya kiti Chake cha enzi cha utukufu. Yeye Ametimiza ukombozi na kuongoza watu Wake wote kuonekana katika utukufu. Yeye hushikilia ulimwengu mikononi Mwake kwa hekima Yake ya uungu na uweza Yeye Amejenga Uyahudi na kuifanya imara. Pamoja na uadhama Wake Yeye huhukumu dunia ya maovu; Yeye huhukumu mataifa yote na watu wote, ardhi na bahari na vitu vyote hai juu yao, pia wale ambao wamelewa kwa divai ya uzinzi.

Ijumaa, 19 Oktoba 2018

Swahili Gospel Video Clip "Maangamizo ya Mungu ya Dunia kwa Mafuriko"


Swahili Gospel Video Clip "Maangamizo ya Mungu ya Dunia kwa Mafuriko"


Unapoitazama dondoo hii ya kustaajabisha ya filamu ya Kikristo Kuangamizwa kwa Dunia kwa Gharika na Mungu, utagundua tabia takatifu, ya haki ya Mungu na utunzaji Wake na huruma kwa wanadamu, na utapata njia ya wokovu wa Mungu katikati ya maafa.

      Kuhusu Sisi: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Alhamisi, 18 Oktoba 2018

Kuhusu Maisha ya Kawaida ya Kiroho


Mwenyezi Mungu alisema, Muumini lazima awe na maisha ya kawaida ya kiroho huu ni msingi wa kupitia maneno ya Mungu na kuingia katika hali halisi. Sasa hivi, je, maombi yote, kule kuja karibu na Mungu, kuimba, kusifu, kutafakari, na kule kujaribu kuelewa maneno ya Mungu ambayo mnatenda yanafikia viwango vya maisha ya kawaida ya kiroho?

Jumatano, 17 Oktoba 2018

Wimbo wa Maneno ya Mungu "Mamlaka na Nguvu Anayoonyesha Mungu Anapopata Mwili"


Mungu alikuja duniani hasa kutimiza ukweli wa "Neno kuwa mwili."
(tofauti na Agano la Kale, katika siku za Musa,
Mungu alizingumza moja kwa moja kutoka mbinguni).
Kisha, yote yatatimizwa katika enzi ya Ufalme wa Milenia
kuwa ukweli ambao watu wanaweza kuona,
ili watu waweze kuona utimizaji hasa kwa macho yao wenyewe.
Hii ni maana ya kina ya Mungu kuwa mwili.
Yaani, kazi ya Roho imekamilika kupitia kwa mwili na neno.
Hii ni maana ya kweli ya "Neno kuwa mwili, Neno kuonekana katika mwili."

Jumanne, 16 Oktoba 2018

209. Mtazamo wa Mungu kwa Mwanadamu


209. Mtazamo wa Mungu kwa Mwanadamu


I
Matendo maovu ya wanadamu yanapomchukiza Mungu,
Ataiteremsha hasira Yake juu yao,
ila wanapotubu kwa kweli mbele Yake.
Watu wanapoendelea kumpinga Mungu,
Ghadhabu Yake haitakoma, hata watakapoangamizwa.
Hii ni tabia ya Mungu.
Kwa maneno mengine, rehema au ghadhabu ya Mungu
inategemea matendo ya mwanadamu na mtazamo wake kwa Mungu. Ah ...

Jumatatu, 15 Oktoba 2018

Tamko la Mia Moja na Tatu

Tamko la Mia Moja na Tatu

Mwenyezi Mungu alisema, Sauti ya mngurumo inatoka, ikiutetemesha ulimwengu mzima, ikiwahanikiza watu, na kuwafanya wachelewe kukwepa, na wengine wanauawa, baadhi wanaangamizwa, na wengine wanahukumiwa. Kweli ni kioja ambacho hakuna yeyote amewahi kukiona awali. Sikiliza kwa makini, milio ya radi inafuatana na sauti za kuomboleza, na sauti hii inatoka kuzimu, sauti hii inatoka jahanamu. Ni sauti yenye uchungu ya wale wana wa uasi ambao wamehukumiwa nami. Wale wasiosema kile Ninachosema na kufanya Ninachokifanya wanahukumiwa vikali na kupokea laana ya ghadhabu Yangu.

2018 Gospel Music "Uumbaji wa Mungu wa Dunia" (Swahili Subtitles)


  Uumbaji wa Mungu wa Dunia


Kitabu cha Mwanzo kimenakili jinsi, hapo mwanzo, Mungu aliuumba ulimwengu kimiujiza. Dondoo hii ya filamu ya Kikristo inakutolea ufanisi wa kushangaza wa Mungu wa kuuumba ulimwengu.

    Kujua zaidi: Kujua Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki Hutoka wapi?

Jumapili, 14 Oktoba 2018

Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu (Sehemu ya Kwanza)


Smiley face


Ni kiasi gani cha kazi ya mwanadamu ni kazi ya Roho Mtakatifu na uzoefu wa mwanadamu ni kiasi gani? Hata sasa, tunaweza kusema kuwa watu bado hawayaelewi maswali haya, ambayo yote ni kwa sababu watu hawaelewi kanuni za utendaji kazi wa Roho Mtakatifu. Kazi ya mwanadamu Ninayoizungumzia, kimsingi, ni kwa kurejelea kazi za wale ambao wana kazi ya Roho Mtakatifu au wale ambao wanatumiwa na Roho Mtakatifu.

Jumamosi, 13 Oktoba 2018

Swahili Christian Music Video | "Ni Watu Waaminifu Pekee Walio na Mfano wa Binadamu" | God Led Me Onto the Right Path of Life



I
Kwa ajili ya faida niliacha viwango vyote vya mwenendo,
na bila haya nikatumia udanganyifu kutafuta riziki yangu.
Sikujali chochote kuhusu dhamiri au maadili, chochote kuhusu uadilifu au heshima.
Niliishi tu kuridhisha tamaa na uroho wangu vilivyozidi kukua.
Kwa moyo usio na amani, nilitembea katika matope ya dhambi,
bila njia yoyote ya kuepuka giza hii isiyo na mipaka.

Ijumaa, 12 Oktoba 2018

Unapaswa Kujua kuwa Mungu wa Vitendo Ni Mungu Mwenyewe

Smiley face



Je, unapaswa kujua nini kuhusu Mungu wa vitendo? Mungu wa vitendo Mwenyewe anajumuisha Roho, Nafsi, na Neno, na hii ndiyo maana ya kweli ya Mungu wa utendaji Mwenyewe. Kama unajua Nafsi pekee—kama unajua tabia na utu Wake—lakini hujui kazi ya Roho, au ambacho Roho hufanya katika mwili, na kuangazia Roho tu, na Neno, na kuomba mbele ya Roho, bila kujua kazi ya Roho wa Mungu katika Mungu wa vitendo, basi hii inadhihirisha kuwa humjui Mungu wa vitendo.

Jumatano, 10 Oktoba 2018

210. Mungu Mwenye Mwili Anapendeza Sana

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

210. Mungu Mwenye Mwili Anapendeza Sana

I
Baada ya Mungu kupata mwili, akiishi maisha kati ya wanadamu,
Aliona upotovu wa mwanadamu, hali ya maisha yake.
Mungu katika mwili alihisi sana kutojiweza kwa mwanadamu,
jinsi gani wanavyodharaulika; Alihisi huzuni yake.

Jumatatu, 8 Oktoba 2018

212. Toa Akili na Mwili ili Kutimiza Agizo la Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Injili

212. Toa Akili na Mwili ili Kutimiza Agizo la Mungu

I
Kama washiriki wa jamii ya wanadamu,
kama wafuasi wa Kristo wa dhati,
ni wajibu wetu, jukumu letu
kutoa akili zetu na miili yetu
kwa kutimiza agizo la Mungu.

Jumapili, 7 Oktoba 2018

213. Wale Ambao Mungu Atawaokoa ni wa Kwanza Kabisa Moyoni Mwake

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

213. Wale Ambao Mungu Atawaokoa ni wa Kwanza Kabisa Moyoni Mwake

I
Kazi ya Mungu ya kuokoa ni muhimu vipi,
muhimu zaidi kuliko vitu vingine vyote Kwake.
Kwa mipango na mapenzi yaliyokusudiwa, sio mawazo na maneno tu,
Anafanya kila kitu kwa wanadamu wote.
Oh ni muhimu kiasi gani, kazi ya Mungu ya kuokoa, kwa ajili ya mwanadamu na Yeye Mwenyewe.

“Sauti Nzuri Ajabu” – Hukumu ya Mungu ya Siku za Mwisho Ni Wokovu kwa Mwanadamu | Filamu za Injili (Movie Clip 5/5)



      Baadhi ya watu husoma maneno ya Mungu na kuona kwamba kunayo mambo makali ambayo ni hukumu ya wanadamu, na shutuma na laana. Wanafikiria kwamba kama Mungu huhukumu na kulaani watu, nao pia hawatashutumiwa na kuadhibiwa? Inawezaje kusemekana kwamba aina hii ya hukumu ni ya kutakasa na kuokoa wanadamu?

Jumamosi, 6 Oktoba 2018

Kuelewa Mapenzi ya Mungu Katikati ya Matatizo

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

13. Kuelewa Mapenzi ya Mungu Katikati ya Matatizo

Xiao Rui    Mji wa Panzhihua, Mkoa wa Sichuan
Nilipokuwa nikihubiri injili nilikutana na viongozi wa madhehebu ambao walisema uongo ili kupinga na kuvuruga, na kuwaita polisi. Hili lilisababisha wale niliokuwa nikihubiria kutothubutu kuwasiliana nasi, na wale ambao walikuwa tu wameikubali injili kutoweza kuwa na imani katika kazi ya Mungu.

Jumatano, 3 Oktoba 2018

Maonyesho ya Mungu "Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili" (Official video)


Mwenyezi Mungu anasema, "Hiyo ni kwa sababu Roho tayari amekwishaanza kazi Yake, na maneno sasa yameelekezwa kwa watu wa ulimwengu mzima. Hii tayari ni nusu ya kazi. Roho wa Mungu amefanya kazi kubwa hiyo tangu dunia ilipoumbwa; Amefanya kazi tofauti katika enzi tofautitofauti, na katika mataifa tofauti. Watu wa kila enzi wanaiona tabia Yake tofauti, ambayo kwa asili inafichuliwa kupitia kazi tofauti Anazozifanya. Yeye ni Mungu, mwingi wa rehema na wema; Yeye ni sadaka ya dhambi kwa ajili ya mwanadamu na mchungaji wa mwanadamu, pia Yeye ni hukumu, kuadibu, na laana kwa mwanadamu. Angeweza kumwongoza mwanadamu kuishi duniani kwa miaka elfu mbili na pia kumwokoa mwanadamu aliyepotoka. Na siku hii, pia Anaweza kumshinda mwanadamu ambaye hamjui na kumfanya awe chini ya utawala Wake, ili kwamba wote wajinyenyekeze kwake kikamilifu. Mwishoni, Atachoma yote ambayo si safi na ambayo si ya haki ndani ya wanadamu katika ulimwengu mzima, kuwaonyesha kwamba Yeye si Mungu wa Rehema, wema, hekima, maajabu na utakatifu pekee, bali pia ni Mungu anayemhukumu mwanadamu."


Tazama Video: Utongoaji wa Neno la Mungu , video za kwaya

Jumanne, 2 Oktoba 2018

Swahili Christian Documentary | "Yule Anayeshikilia Ukuu Juu ya Kila Kitu" (Official Video)



Kote katika ulimwengu mkubwa mno, sayari zote ya mbingu husogea kwa usahihi katika mizunguko yazo zenyewe. Chini ya mbingu, milima, mito, na maziwa vyote vina mipaka yavyo, na viumbe vyote huishi na kuzaana wakati wa misimu yote minne kulingana na sheria za maisha…. Hili lote limepangwa vizuri sana—je, kuna Mwenye Uwezo Mmoja anayepanga na kutawala yote haya?

Jumatatu, 1 Oktoba 2018

Tamko la Themanini na Nne


Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mwenyezi Mungu

Tamko la Themanini na Nne

Kwa sababu ya ukosefu wao wa ujuzi kunihusu Mimi, mwanadamu amekatiza usimamizi Wangu na kudhoofisha mipango Yangu mara zisizo na idadi, lakini hawajawahi kuweza kuzuia hatua Zangu zinazoendelea mbele. Hii ni kwa sababu Mimi ni Mungu wa hekima. Pamoja na Mimi kuna hekima isiyo na mipaka; pamoja na Mimi kuna siri isiyo na mipaka na isiyoweza kueleweka. Mwanadamu hajawahi kuweza kuielewa na kuifahamu kabisa tangu zamani za kale hadi milele.